Misikiti minane kufungwa Tunisia
Utawala nchini Tunisia unasema kuwa utafunga misikiti minane wiki moja inayokuja kwa madai kwa inachochea ghasia.
Hii
ni kufuatia shambulizi lililofanyika kwenye hoteli moja ambapo watu 39
wengi wao wakiwa raia wa kigeni waliuawa na mwanamme mmoja aliyedanganya
kuwa mtalii.Kundi la islamic state lilisema kuwa ndilo lililotekeleza shambulizi hilo.
Waziri mkuu nchini Tunisia Hanib Essid anasema kuwa baadhi ya misikiti ilikuwa ikitumika kueneza propaganda na kuunga mkono ugaidi.
chanzo:bbcswahili
0 comments: