Waalimu wa madrasa wakuhumiwa jela

...................

Waalimu wa madrasa wakuhumiwa jela Uingereza

Waalimu wawili wa shule ya Madrasa, ambao walimuadhibu mtoto mmoja mwenye umri wa miaka 10, kwa kumpiga viboko, baada ya kumtuhumu kutosema maandishi ya Koran kikamilifu wamehukumiwa kifungo cha jela cha mwaka mmoja.
Mohammed Siddique, mwenye umri wa miaka 60, na mwanawe wa kiume Mohammed Waqar, mwenye umri wa mika 24, walikiri kosa hilo la kumdhulumu mtoto wa chini ya umri wa miaka 16 kimakusudi.
Wawili hao wanatuhumiwa kutekeleza ukatili huo katika msikiti wa Jamia iliyoko eneo la Sparkbrook, mjini Birmingham, Uingereza kati ya mwezi Mei na Juni mwaka huu.
Mahakama hiyo pia imewapiga marufu wawili hao kufundisha mafundisho yoyote ya kidini.
Mwendesha mashtaka, aliiambia mahakama hiyo kuwa mtoto huyo alipigwa kwa kutumia plastiki na pia kuzabwa makofi na waalimu wake, kwa madai ya kuzungumza akiwa darasani, katika kituo hicho cha mafundisho ya Kiislamu.
Mahakama ilionyesha picha za mtoto huyo alidhulumiwa mara kadhaa na pia majeraha aliyoyapata.
Upande wa mashtaka ulisema mtoto huyo kwa sasa ametatizika kiakili na hata kwa sasa hataki kwenda msikitini.
Wakili wa washukiwa hao Charanjit Jutla, aliiambia mahakama hiyo kuwa wawili hao ni watu wenye rekodi ya kuwa na tabia nzuri na wamejuta matendo yao.

chanzo:bbcswahili
http://3.bp.blogspot.com/-e0QpO-QtZzE/U5DWDUZasXI/AAAAAAAABWg/QlFF97gwNdc/s1600/RAHA+GIF.gif
GIVE YOUR OPINIONS HERE

0 comments: