WASHABIKI WA SIMBA MNATAKIWA KUJUA JAMBO HILI.......JUU YA TIMU YENU
Mechi Tano ngumu za Simba mzunguko wa Kwanza wa Ligi Kuu
Simba na kati ya timu tatu kubwa zinazopewa nafasi kubwa ya kufanya
vizuri kwenye msimu mpya wa Ligi ya Vodacom unaotarajia kuanza Septemba
12 na hiyo inatokana na usajili inaoendelea kuufanya baada ya kufanya
vibaya kwenye misimu mitatu iliyopita.
Ratiba inaonyesha Simba msimu huu itaanza ugenini kwenye uwanja wa
Mkwawani ikipambana na timu ya Africans Sports inayoshiriki kwa mara ya
kwanza baada ya miaka 23, kupita tangu ishuke daraja lakini mchezo huo
wa Septemba 12 hauonekani kuwa kikwazo kwa Simba kulingana na uwezo
waliokuwa nao wapinzani wao kazi kubwa itakuwa Septemba 16 kwenye uwanja
huohuo wa Mkwakwani Tanga ambapo Simba itapambana na Mgambo JKT .
Huo ni mchezo mgumu kwa kocha Muingereza wa Simba Dylan Kerr ambaye
atakuwa na kazi kubwa ya kuweka rekodi mpya ya kuondoka na ushindi
kwenye uwanja huo dhidi ya Mgambo JKT ambayo imekuwa na rekodi nzuri ya
kuifunga Simba kila wanapokutana kwenye mchezo huo.
Mchezo mwingine mgumu kwa Simba utapigwa Septemba 26 dhidi Kagera
Sugar kwenye uwanja wa taifa Dar es Salaam na mtihani mwingine mkubwa
pengine kuliko yote kwa Simba ni Septemba 26 wakati watakapo kutana na
wapinzani wao wa jadi Yanga kwenye uwanja huo wa taifa.
Baada ya hapo kikosi cha kocha Kerr kitasafari hadi Mbeya ambapo
Oktoba 17 itakuwa na kibarua kipevu kwenye uwanja wa Sokoine kwa
kupambana na Mbeya City timu ambayo imekuwa ikiisumbua sana Simba tangu
ilipoanza kushiriki Ligi ya Vodacom msimu miwili iliyopita.
Msimu uliopita Mbeya City ilichukua pointi zote sita kwa kushinda
mechi zote mbili za nyumbani na ugenini na hiyo ndiyo itakayofanya
mchezo kati ya timu hizo mbili kuwa mgumu na wenye ushindani mkubwa.
Novemba 7 Simba itakuwa ikipambana na Azam timu ambayo imekuwa na
uhasama nayo tangu kumalizika kwa msimu uliopita na hii inatokana na
timu hizo kukamiana kila zinapokutana na msimu uliopita zilipokutana
Simba aliambulia pointi moja na Azam iliyokuwa chini ya kocha Joseph
Omog na Georg Nsimbe ‘Besti ilivuna pointi nne.
chanzo:goal.com
0 comments: