MABOMU YALINDIMA SONGEA, WATU WANNE WASHIKILIWA KWA KUJARIBU KUTEKA MAGARI YALIYOBEBE VIFAA VYA KUPIGIA KURA

...................


Jeshi la polisi mkoa wa Ruvuma linamshikiria mtu mmoja ambaye inadaiwa ni mfuasi wa CHADEMA wa manispaa ya Songea na linawasaka watu wengine ambao ni wafuasi wa chama hicho ambao wanadaiwa walisababisha kufanya maandamano yasiyo rasmi yaliyopelekea kuwepo vurugu na kufunga barabara ya kutoka songea kwenda Mbinga ambapo baadae polisi walilazimika kutumia mabomu kutawanya maandamano hayo.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma mihayo msikhela aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 12 jioni huko katika eneo la lizaboni manispaa ya Songea ambapo wafuasi wa CHADEMA mara baada ya kumaliza mkutano wakufunga kampeni waliamua kuanzisha maandano ambayo yalikuwa hayana kibali.

Alisema kuwa maandamo hayo yalianza kwenye eneo walilokuwa wakifanyia mkutano na kuelekea Songea mjini huku wakiwa wameongozana na mgombea ubunge kupitia chama hicho Joseph Fuime ambapo baadae walitakiwa watawanyike lakini walikaidi amri halali ya jeshi la polisi.

Kamanda Msekhela alifafanua zaidi kuwa baada ya wafuasi hao kutotii amri hiyo jeshi la polisi lililazimika kutumia nguvu kutawanya maandamano hayo, kutokana na wafuasi wa chama hicho kuanzisha vurugu kwenye eneo hiyo walilokuwa wakipita na kusababisha kufunga barabara kuu iendayo wilaya ya Mbinga na Nyasa.

Alisema kuwa wafuasi hao pia kufautia tukio hilo wamewajeruhi askari polisi wanne kwa kuwashushia vipigo sehemu mbalimbali za miili yao na majina yao yamehifadhiwa na kwamba inadaiwa askari hao walishambuliwa kwa mawe na baadae gari la polisi lilipofika eneo la tukio na kuwataka wafuasi hao watawanyike kwa amani bado waliendelea kuonesha kutotii amri ya polisi.

Alieleza zaidi kuwa kufuatia vurugu hizo jeshi la polisi mkoani humu linamshikiria mtu mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa ambaye anadaiwa ndiye alianzisha kuwarushia mawe askari ambao kwasasa hizi wanaugulia majeraha.

Kamanda Msekhela alisema kuwa kwasasa hivi polisi inaendelea kufanya upelelezi wa kina ikiwa ni pamoja na kumtafuta mgombea ubunge kupitia CHADEMA Fuime ili aweze kutoa maelezo yakinifu ni kwa nini waliamua kufanya maandamano, na kwamba upelelezi huo utakapo kamilika mtuhumiwa huyo anayeshikiliwa na polisi atafikishwa mahakamani kujibu shitaka linalomkabili.
 
WAKATI HUO HUO, watu wanne wanashikiliwa na polisi katika kituo cha polisi wilaya ya Mbinga kwa jaribio la kutaka kuteka magari yaliyokuwa yamebeba vifaa vya kupigia kura yakiwemo masanduku kura kwenye eneo la Darpori wilayani Nyasa.

Alisema kuwa wakiwa kwenye magari hayo maafisa wa serikali walishituka kuwekewa vizingiti barabarani na waliposimama watu hao walitoka porini wakiwa wameshika mapanga na silaha nyingine za jadi, ndipo kwa ukakamavu wa hali ya juu  askari polisi ambao walikuwa na silaha nzito walishuka na kupambana nao kisha kuwatia nguvuni
 
Chanzo: http://kazimoja.blogspot.com


http://3.bp.blogspot.com/-e0QpO-QtZzE/U5DWDUZasXI/AAAAAAAABWg/QlFF97gwNdc/s1600/RAHA+GIF.gif
GIVE YOUR OPINIONS HERE

0 comments: