KAZI IMEANZA, KWELI HAPA KAZI TU
Katibu
 Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru akikagua mabegi 
matano yenye Kobe 201 yaliyokamatwa usiku wa kuamkia leo na askari 
wanyamapori kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama katika 
uwanja wa Kimataifa wa J.K. Nyerere jijini Dar es Salaam.  
Watuhumiwa
 hao wa usafirishaji wa wanyamapori wametajwa kuwa ni David Mungi mkazi 
wa Muheza Mkoani Tanga na Mohammed Suleiman (43) mkazi wa Zanzibar ambao
 katika tukio hilo walishafanikiwa kupita kwenye mitambo ya ukaguzi 
lakini mbwa maalum (sniffer dogs) wakasaidia kugundua uhalifu huo. Kwa 
pamoja watuhumiwa hao walikamatwa na tiketi za kusafiria kuelekea nchini
 Malaysia. 

Kobe
 wapatao 201 waliokamatwa na askari wanyamapori kwa ushirikiano na 
vyombo vya ulinzi na usalama kwa kutumia mbwa maalum (sniffer dogs).   

Kaimu
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Maliasili na 
Utalii Bi. Dorina Makaya kulia na Mmoja wa Askari wanyamapori 
wakiangalia kobe 103 waliotelekezwa eneo la Tabata hivi karibuni baada 
wahalifu waliohusika kuhofia kukamatwa na vyombo vya dola. (Picha na Hamza Temba - Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Maliasili na Utalii
chanzo: matukiotz.co.tz

0 comments: