WALIOFUKIWA NA KIFUSI MGODINI SIKU 41 ZILIZOPITA WANENA HAYA
Mmoja wa wahanga hao akiwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama. 
Katika 
hali isiyokuwa ya kawaida watu 5 kati ya 6 waliyokuwa wamefunikwa na 
kifusi kwa siku 41 katika machimbo madogo wa nyangalata wilayani kahama 
mkoani shinyanga wameokolewa wakiwa hai. 
Wakizungumza
 leo na kahama fm wakati wakiwa wamelazwa katika hospitali ya mji wa 
kahama, wahanga hao wamesema hali hiyo imewakuta katika harakati za 
kuwaokoa wenzao waliokuwa wamefukiwa na kifusi katika machimbo hayo. 
Wahanga 
hao ni Onyiwa Kanyimbo(55),Msafiri Jerald(38) Amosi Muhangwa(25), Chacha
 wambura(53) na Joseph Burule(44) na aliyefariki dunia ni Mussa Supana. 
Wamesema 
walikuwa wakiishi kwa kunywa maji, na kula magome ya miti pamoja na 
mende hali iliyowasababisha kuendelea kuwa hai kwa siku 41 hadi jana 
jioni walipookolewa. 
Menaja wa
 mgodi mdogo huo Amosi Mbanga amesema timu ya mafundi ilifanya utafiti 
na kugundua kuna sauti za watu zikiita na kuamua kupeleka uwokawaji 
kushirikiana na serikali pamoja kampuni acaica na kufanya uokowaji huo 
ulichukua masaa 24. 
Naye 
kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya kahama Dk. Jibai Mkama 
amethibitisha kuwapokea wahanga hao na kwa sasa hali zao zinaendelea 
vizuri wakiwa bado wanapatiwa matibabu katika hosspitali hiyochanzo: matukiotz.co.tz


0 comments: