Mbwa ‘shujaa wa Paris’ avuma mtandaoni
Katika vita, huwa kuna watu wanaoibuka mashujaa na kuenziwa na watu na taifa kwa jumla.
Huko
Ufaransa, kuna mbwa mmoja wa polisi ambaye amepata umaarufu mkubwa sana
na kusifiwa baada yake kufariki kwenye operesheni ya polisi.Mbwa huyo wa jina Diesel anaweza kuelezwa kuwa ‘afisa wa polisi’ wa kwanza kufa vitani katika operesheni dhidi ya washukiwa walioshambulia Paris Ijumaa.
Kuna hata ukurasa uliofunguliwa kwenye Twitter wenye jina lake na mada hiyo 'Je Suis Chien'
Kwenye Twitter, habari za kuuawa kwa mbwa huyo wa umri wa miaka saba na "magaidi” zilisambazwa zaidi ya mara 13,000.
Aliyeanzisha kitambulisha mada hicho anasema alikuwa akifanya mzaha tu.
Ashley, 24 anayeishi karibu na Paris alisema: “Nilitaka kuwe na mzaha kiasi kwa sababu tovuti karibu zote zilikuwa zinazungumzia hili”.
Aliambia BBC Trending kwamba alianzisha kitambulisha mada hichi ili pia kufanyia mzaha kuenea kwa vitambulisha mada vya"Je Suis...". "Kila tatizo likitokea kuna #JeSuis," amesema.

0 comments: