Mzaha wamtia mashakani rais wa Bolivia

...................


Rais wa Bolivia Evo Morales ameomba msamaha kwa kufanya mzaha kuhusu uwezekano wa waziri wake wa afya Ariana Campero kuwa mpenzi wa jinsia moja.
Amesema kuwa hakuwa na lengo la kumkosea mtu yeyote na kwamba anaheshimu jinsia zote.
Bi Campero ambaye ni daktari wa mika 29 amekuwa akikabiliwa na matmshi kama hayo kutoka kwa wanasiasa wakuu nchini Bolivia.
Bwana Morales alutoa matamshi hayo wakati wa sherehe rasmi ya kiserikali katika mkoa wa kaskazini wa Beni.
Aligundua bi Campero alikuwa akizungumza na mwanamke mwengine wakati alipkuwa akitoa hotuba yake na kwamba hakuwa akimsikiliza.
Bwana Morales aliingilia kati mazungumzo hayo na kusema:''Sitaki kudhania kuwa wewe ni mpenzi wa jinsia moja,Nisikilize vizuri,nenda ukaolewe!''Matamshi yake yalizua hisia kali kutoka kwa wapenzi wa jinsia moja katika taifa hilo.
Na iwapo waziri huyo alikuwa mpenzi wa jinsia moja tatizo ni lipi? Lilihoji kundi moja la wanawake ambao ni wapenzi wa jinsia.
Bwana Morales alitoa taarifa akisema kuwa ameomba msamaha ''kwa unyenyekevi na dhati iwapo alimkosea mtu yeyote,akiongezea kuwa :tunaheshimu jinsia tofauti na hilo liko wazi katika katiba yetu.
Bolivia ina sheria ya usawa wa kijinsia na wanwake wengi wanashikilia nyadhfa muhimu za kisiasa

chanzo:bbcswahili
http://3.bp.blogspot.com/-e0QpO-QtZzE/U5DWDUZasXI/AAAAAAAABWg/QlFF97gwNdc/s1600/RAHA+GIF.gif
GIVE YOUR OPINIONS HERE

0 comments: