WATU ZAIDI YA 20 WAUAWA, RAIS ATANGAZA HALI YA HATARI
Bw keita ametangaza hali ya hatari itakayodumu kwa siku 10, pamoja na siku tatu za maombolezo ya kitaifa.
Watu
 wenye silaha wanaodaiwa kuwa wanamgambo wa kundi la Kiislamu 
walishambulia hoteli ya Radissom Blue mjini Bamako na kushikilia mateka 
watu 170.
Maafisa wa Marekani wamethibitisha hakuna mateka zaidi wanaoshikiliwa.
Makundi ya Al-Qaeda Afrika Kaskazini na kundi jingine la al-Murabitoun yamedai kuhusika kwenye shambulio hilo.
Baraza kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa limeshutumu shambulio hilo.
Akiongea
 baada ya mkutano wa dharura wa baraza la mawaziri, Rais Keita alisema 
watu 21 waliuawa kwenye shambulio hilo, wakiwemo washambuliaji wawili.
Image copyrightReutersImage captionWanajeshi wa Ufaransa walisaidia katika operesheni hiyo
Ripoti
 za awali zilikuwa zimesema watu 27 waliuawa. Afisa wa UN, ambaye 
hakutaka jina lake litajwe, alisema miili 12 ilipatikana ghorofa ya 
chini ya hoteli hiyo na miili 15 ghorofa ya pili.
Mmoja wa mateka waliouawa ni Geoffrey Dieudonne, mbunge aliyewakilisha jimbo la Wallonia nchini Ubelgiji.
Shirika
 la habari la serikali ya Uchina Xinhua linasema raia watatu wa Uchina 
ni miongoni mwa waliouawa. Marekani nayo ilisema raia wake mmoja 
aliuawa.
Waziri wa mashauri ya kigeni wa Uingereza Philip Hammond alisema Waingereza watatu waliokuwa hotelini humo wako salama.
Hoteli hiyo inamilikiwa na Wamarekani na hupendwa sana na raia wa kigeni.
Image copyrightReutersImage captionHoteli ya Radisson Blu hupendwa sana na wageni
Watu
 walioshuhudia shambulio hilo walisema wapiganaji hadi 13 waliingia 
kwenye hoteli hiyo wakiimba "Mungu ni Mkubwa!” kwa Kiarabu.
Kabla
 ya vikosi maalum kuingia humo, mdokezi mmoja aliambia shirika la habari
 la Reuters kwamba baadhi ya mateka walioweza kukariri vifungu vya Koran
 waliachiliwachanzo:matukiotz.co.tz
0 comments: