YAWEZEKANA HII NI NJIA RAHISI YA KUVUNJA MAHUSIANO
Je,unataka kuvunja uhusiano wako kwa urahisi?
Hakuna hisia mbaya
zaidi inayokujia wakati unapokutana na chapisho linalokuhusisha wewe na
mpenzi wako wa zamani mukijifurahisha.
Ni vibaya zaidi unapogundua kwamba jina la pili la mpenzi huyo wa zamani limebadiliswa.Hatahivyo kuna habari njema,mtandao wa facebook umetangaza kuwa unatafuta mbinu mpya ya kupunguza machungu unayopata wakati unapokutana na mpenzi wa zamani ambaye muliwachana baada ya ugomvi.
Kwa sasa,iwapo hutaki kukumbushwa kuhusu mpenzi huyo wa zamani una uwezo wa kumuondoa kama rafiki ama hata kumzuia asiweze kukuona katika mtandao wa facebook.
Tatizo ni kwamba watajua kwamba umechukua hatua kama hiyo ambayo sio nzuri sana.
Mahusiano katika mtandao wa facebook ni swala muhimu sana,kama alivyosema jaji mmoja kutoka mjini New York, kwamba unaweza kutuma wito wa talaka katika mtandao huo na uwe halali.
Lakini kifaa kipya cha mtandao wa facebook kinalenga kubadilisha kile ambacho mpenzi wako wa zamani anaweza kuona,bila kujua kwamba kuna kitu umefanya..
Kipengele hicho kinaruhusu:
*Kutoliona mara kwa mara jina la mpenzi wa zamani pamoja na picha yake bila kuiondoa ama kumzuia kukuona.
*Machapisho yao hayataonekana na majina yao hayatorodheshwa wakati watu wanapoandika ujumbe mpya ama hata kuwasambazia marafiki picha zao.
*Zuia picha ,video ama hata machapisho yoyote ambayo mpenzi wako wa zamani anaweza kuyaona.
*Weka usimamizi wa ni nani anayeweza kuona picha zako na mpezi wako wa zamani na uziondoe katika machapisho yenu pamoja.
*Wakati facebook ilipozinduliwa katika taasisi na vyuo vikuu,lengo lake lilikuwa machapisho ya mahusiano.Ni hatua ya kidijitali ambayo ilisaidia mda wa wengi.
Lakini hivi majuzi,watu wamekuwa wakichukua tahadhari wanapotangaza uhusiano wao katika facebook.
Watu walikuwa wakitumia neno ''its complicated'' kwa uhusiano ambao unaelekea kugonga mwamba na badala yake watu wanatumia maneno ya kidunia kama vile 'kuchumbiwa' ama hata 'kupata mtoto'.
Hatahivyo kifaa hicho kipya kitaanza kutumika hivi karibuni,imesema facebook.
Mpango huo ni mongoni mwa juhudi zinazoendelea kuendeleza raslimali za watu wanaokabiliwa na wakati mgumu katika maisha yao,aliandika Kelly Winters meneja msimamizi wa bidhaa za facebook.
''Tunaamini kifaa hicho kitawasaidia watu kumaliza uhusiano wao katika facebook kwa urahisi na udhibiti.Iwapo unatumia simu ya mkononi nchini Marekani unaweza kukitumia kifaa hicho mara moja kwa kuvunja uhusiano na mpenzi wako''
chanzo:bbcswahili
0 comments: