JIFUNZE KUHUSU UGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBO

...................


 Image result for picture of a man in pain from stomachImage result for picture of a man in pain from stomachImage result for picture of a man in pain from stomach
Karibu sana mpendwa msomaji wa makala zangu mbalimbali za afya uwezekujifunza huenda ukawa unafahamu ila sio vibaya kujimbusha na wewe ambae haufahamu utakuwa ni wasaa wako mzuri kabisa wa kujifunza baadhi ya mambo leo tuangalia zaidi ugonjwa wa VIDONDA VYA TUMBO katika mambo haya:-
1.Visababishi vya vidonda vya tumbo
2.Dalili za vidonda vya tumbo
3.Madhara ya ugonjwa wa vidonda vya tumbo
Vidonda vya tumbo ni ugonjwa unaosumbua watu wengi kote duniani na mara nyingine kupelekea vifo vya watu.Kuna aina nne za vidonda vya tumbo ila hizi tatu ndio husumbua sana
-Vidonda vinavyotokea kwenye mfuko wa kuhifadhia chakula (Grastric ulcers)
-Vidonda vinavyotokea kwenye sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo (doudenal ulcers)
-Vidonda vinavyotokea kwenye koo (oesophagel ulcers)
Vitu vinayosababisha vidonda vya tumbo ni kama zifuatavyo
1.Mawazo kupita kiasi (strees)
2.Kupenda kula vitu vyenye asidi kwa wingi kama limao,pilipili na nk
3.Uvutaji wa sigara na unywaji wa pombe kupita kiasi
4.Maradhi ya Ini
5.Ulaji wa chakula usiokuwa na mpangilio maalumu
Dalili za ugonjwa huu ni hizi zifuatazo
1.Maumivu makali
2.Kiungulia maeneo ya chembe moyo epigastic pains
3.Maumivu juu kidogo ya tumbo mara nyingi huendana na muda wa kula chakula
3.Mtu mwenye vidonda kwenye utumbo anapata maumivu makali sana kipindi anapokula au mara tu baada ya kumaliza kula wakati mtu aliye na vidonda kwenye sehemu ya kwanza ya tumbo hupata maumivu makali anapokuwa na njaa na hupata nafuu pindi anapokula.
4.Kutapika damu
5.Kupoteza hamu ya kula na kupungua uzito
6.Kuvimbiwa au tumbo kujaa gesi
7.Kucheua na kuongezeka kwa mate yanayoshuka tumboni baada ya kucheua
8.Kupata haja kubwa yenye rangi nyeusi au kahawaia chenye harufu mbaya sana.
Hivyo basi kama unadalili hizo hapo ni vema ukafika kituo cha afya au hospitali kwa ajili ya vipimo na kuanza matibabu
Tafadhali kama unamaoni au ushauri usisite kuniandikia kwenye namba 0758190516 karibuni sana



http://3.bp.blogspot.com/-e0QpO-QtZzE/U5DWDUZasXI/AAAAAAAABWg/QlFF97gwNdc/s1600/RAHA+GIF.gif
GIVE YOUR OPINIONS HERE

0 comments: