Coleen Rooney kula kondo la nyuma

...................

Coleen
Mke wa nahodha wa Manchester United Wayne Rooney, Coleen Rooney, ametangaza kwamba atakula kondo lake la nyuma baada ya kuzaliwa kwa mwana wao wa tatu aliyepewa jina Kit.
Kondo hilo la nyuma, limetengenezwa na kuwa vidonge na anasema amekabidhiwa vikiwa vimewekwa kwenye jagi.
Vidonge hivyo vimeandaliwa na “mtaalamu wa kugeuza kondo la nyuma kuwa vidonge”, anayesema kumeza vidonge hivyo humsaidia mwanamke aliyejifungua kurejelea hali yake ya kawaida haraka.
Mwingine aliyewahi kufanya hivyo awali ni Kim Kardashian, aliyekula kondo lake la nyuma baada ya kujifungua mtoto wake wa kwanza North West.
Mwigizaji wa Mad Men January Jones pia alikula kondo lake la nyuma baada ya kujifungua mwanawe wa kiume Xander mwaka 2011.

Hata hivyo, Coleen ameandika kwenye Twitter kwamba haigi Kim na kwamba hakuwa amesikia kuhusu mwigizaji huyo.
Coleen alijifungua mtoto wake wa tatu wa kiume Jumapili.
Ana watoto wengine wawili wa kiume: Kai naKlay.
Wengine waliowahi kula kondo la nyuma ni mwigizaji wa Clueless Alicia Silverstone made na Kourtney Kardashian aliyemfuata dada baada ya kujifungua mwanawe wa tatu 2014

chanzo:bbcswahili
http://3.bp.blogspot.com/-e0QpO-QtZzE/U5DWDUZasXI/AAAAAAAABWg/QlFF97gwNdc/s1600/RAHA+GIF.gif
GIVE YOUR OPINIONS HERE

0 comments: