JE HILI LINAUKWELI...?

...................


UMEWAI KUHISI KUKABWA USIKU USINGIZINI??,SOMA HAPA ILI USIKABWE TENA
Watu wengi huzani hukabwa usiku na wachawi na mara nyingi wengine huamua hata kwenda kuwaonya watu ambao wanawahisi waliwakaba usiku ndotoni.
Ukweli ni kwamba hakuna anaekukaba ndotoni.
Watu wengi hufikiri kwamba anayewakaba ni Jini lakini Tendo hilo kwa kitaalamu linajulikana kama Mwili kupooza katika usingizi (Sleeping Paralysis)
Tendo hilo huwa linakutokea katika muda wa sekunde 20 lakini wewe unayehusika utahisi kama dakika 5 au dakika 10.
Matukio hayo ya kijinamizi yanatofautiana na yanakutokea wakati ukiwa nusu usingizini na nusu macho.
Ukweli ni kwamba hayana madhara yoyote, ila yanakupa khofu kwa muda fulani.
Unapokabwa unakuwa na fahamu nusu. Unaweza kufungua macho, na utahisi kupiga kelele lakini watu hawakusikii, Mwili wako unakuwa hauwezi kufanya lolote na viungo vya mwili wako vinakuwa havifanyi kazi.
Kitaalamu binadamu anapolala usingizi viungo vyote vya mwili vinakuwa havifanyi kazi,moyo na ubongo pekee ndio huendelea na kazi zake,na ubongo ndio haswa huendelea na kaz zake na ikumbukwe UBONGO NDIO HUTUNZA KUMBUKUMBU ZOTE ZA BINADAMU.
Mawazo ndio sababu kuu ya kukabwa na jinamizi,ubongo ambao ndio uhifadhi kumbukumbu zako ndio huchochea hali hii,na hali hii huchochewa na kitendo cha kulala chali yaani ukilala huku unaangalia juu.
Ndoto mojawapo ambayo watu wengi huota ni kukimbizwa na watu au mtu na unakuwa unapiga kelele lakin sauti haitoki,inapotokea unakimbizwa na watu mara nyingi unakuwa katika mawazo mengi ya kimaisha na hapo kunakuwa na jambo baya linalokusumbua na unakuwa unalikimbia pasipo kulikabili,pia unaweza kuota unauliwa au kifo na n.k,mawazo yako yote hubaki kwenye kumbu kumbu ya ubongo na baadae ubongo unapojifikilisha mwili wako unakuwa umepoa kwa usingizi na viungo havifanyi kazi.
JINSI YA KUZUIA KUKABWA NA JINAMIZI
1.Ikikutokea hali hiyo jaribu kuvuta pumzi nyingi ndani kwa sababu pumzi peke yake ndio unayoweza kuidhibiti ukiwa umekabwa.
2.Jiepushe kulala chali.
3.Punguza mawazo mengi.
4.Lala katika muda mzuri na jaribu kupata muda mrefu wa usingizi masaa 8 mpaka
5.Jaribu kuwa na muda maalum wa kulala ikiwa ni saa 3 basi iwe muda huo wakati wote.
6.Jaribu kula vizuri kabla hujalala.
7.Kumbuka kwamba pamoja ya kuwa hali hii inatisha lakini haina hatari yoyote.
8.Ukihisi unakabwa jaribu sana kujitingisha, hali ya kukabwa itakwisha.
9.Ukiona kama unataka kukabwa amka kaa chini kwa dakika 5 halafu lala tena.
Kumbuka ili kuzuia hali hii hunabudi kulala ukiwa umemaliza migogoro isiyo na ulazimu inayokukabili.PIA HUWEZI KUKABWA NA JINAMIZI KAMA HUNA MAWAZO
Imeletwa kwenu na:-
ISSA MSURI
http://3.bp.blogspot.com/-e0QpO-QtZzE/U5DWDUZasXI/AAAAAAAABWg/QlFF97gwNdc/s1600/RAHA+GIF.gif
GIVE YOUR OPINIONS HERE

0 comments: