TOKA MLOWO-SONGWE:Polisi yataka kususiwa chakula cha msibani
kamanda wa polisi mkoa wa songwe akiongea na wananchi kutatua mgogoro huo
Na Saimeni Mgalula,Songwe
Hali ya uvunjifu wa amani ilitanda katika mji mdogo wa mlowo
wilayani Mbozi Mkoani songwe,Baada ya wananchi kuchoma moto magurudumu ya
magari katika barabara itokayo mkoa wa Mbeya kwenda Tunduma mkoani hapa.
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea majira ya mchana Agost 28 mwaka huu
baada ya wananchi wa Mlowo kudai kuwa mkazi mmoja aliyefahamika kwa jina la
Stanslaus Kalinga (42) kupigwa na Askari baada ya kukamatwa kwa kosa la uzembe
na uzururaji. Marehemu alifia katika hospitali ya Wilaya ya Mbozi akipatiwa
matibabu.
Naye Diwani wa Kata ya Mlowo Sebastian Kilindu alikiri
kutokea kwa tukio hilo na baadaye alikwenda Polisi ili kupata ukweli wa tukio
hilo kuwa je ni kweli polisi wamejihusisha na tukio hilo ili aweze kubaini
ukweli huo.ambapo aliambiwa askari hawajajihusisha na tukio hilo.
Akithibitisha tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa songwe
Mathias Nyange alisema kuwa jeshi la polisi lilimkamata marehemu huyo na
hakupigwa na polisi kama inavyodaiwa kwani taarifa kamili juu ya kifo hivyo
nitaitoa baada ya uchunguzi wa Daktari
Katika hali isiyo ya kawaida wakazi wa Mlowo walibeba
chakula kutoka msibani na kukipeleka kituo cha Polisi Mlowo wakiwa hawana ukeli
wa kifo cha marehemu ambacho kilisababishwa na Askari hivyo nao washiriki kula
chakula hicho.
0 comments: