RAIS WA ZIMBABWE: MAJAJI WAMEFANYA UZEMBE KURUHUSU MAANDAMANO YA UPINZANI
Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amewatuhumu
majaji wa mahakama za nchi hiyo kuwa wazembe kwa kuruhusu maandamano ya
kupinga serikali ambayo baadaye yaligeuka kuwa ya fujo na machafuko.
Mugabe alitoa matamshi hayo jana katika mkutano wa tawi la
vijana la chama tawala cha ZANU-PF, siku mbili kabla ya Mahakama Kuu
kusikiliza shauri la kupinga uamuzi uliotolewa wiki iliyopita wa kupiga
marufuku rasmi maandamano ya upinzani.Serikali ya Zimbabwe ilichukua uamuzi wa kupiga marufuku kwa muda wa wiki mbili maandamano yote katika mji mkuu Harare ambao umekuwa ukishuhudia maandamano ya kulalamikia utendaji wa Rais Mugabe katika kushughulikia matatizo ya uchumi, uhaba wa fedha na ukosefu wa ajira nchini humo.
Kwa mujibu wa gazeti hilo Mugabe amesema mahakama, mfumo wa sheria na majaji wa Zimbabwe wanapaswa kuwa watu wenye uelewa zaidi kuliko raia wa kawaida na kwamba wasizembee katika maamuzi wanayotoa wakati yanapowasilishwa maombi na watu wanaotaka kuandamana.

0 comments: