ADHABU HII IKITOLEWA TZ UTAIPOKEA KWA MTAZAMO GANI...?

...................

Miaka 10 jela kwa wadanganyifu wa mitihani Kenya

Wanafunzi watakaofanya udanganyifu wa mitihani kupewa adhabu ya miaka 10 jela nchini Kenya

Miaka 10 jela kwa wadanganyifu wa mitihani Kenya
Baraza la taifa la mitihani Kenya (KNEC) limetangaza hatua kali na adhabu ya miaka 10 jela kwa wanafunzi watakaofanya udanganyifu wa mtihani .
Tangazo hilo limefanyika wakati ambao wanafunzi wa darasa la nane kote nchini wanatarajiwa kufanya mtihani wa kitaifa wa KCPE mnamo mwezi Novemba .
Aidha miongozo kwa ajili ya mitihani ya kitaifa ya shule za Sekondari (KCSE)  na ya shule za msingi (KCPE) imeweka shilingi bilioni 2 kama faini wa wahusika wowote wa udanganyifu huo wa mitihani .
Sheria zaidi kuhusu suala hilo la udanganyifu ni kuwa yeyote atakayepatikana akifanya mtihani kwa niaba ya mwanafunzi aliyesajiliwa atapata adhabu ya miaka 2 jela au faini ya shilingi milioni 2 au zote,huku kwa wale watakaoharibu vifaa vya mitihani kupata faini ya shilingi milioni 5 au miaka 5 jela .
Hatua hizo kali ni sehemu ya mageuzi na KNEC yenye lengo la kurejesha uaminifu wa mitihani ya taifa ambayo imedhoofika katika miaka ya hivi karibuni
http://3.bp.blogspot.com/-e0QpO-QtZzE/U5DWDUZasXI/AAAAAAAABWg/QlFF97gwNdc/s1600/RAHA+GIF.gif
GIVE YOUR OPINIONS HERE

0 comments: