DARASA ASEMA...ETI AMEWAHI KWENDA KWA MGANGA WA KIENYEJI: KILICHOMPELEKA HIKI HAPA (VIDEO)
Msanii wa bongofleva Darassa
ambaye jina lake limeongoza kwa kutajwa mara nyingi kwenye namba kubwa
za chati za Radio/TV Tanzania kutokana na hit single ya ‘muziki‘ amekaa kwenye Exclusive Interview na Diva kwenye Ala za Roho CloudsFM.
Diva amemuuliza Darassa maswali
mbalimbali ikiwemo ya maisha yake ya kimapenzi na maisha ya mtaani kwa
ujumla ambapo Darassa amekiri kwamba aliwahi kwenda kwa mganga wa
kienyeji ili kutafuta suluhisho la maisha aliyokua anayapitia.
Amesema ‘Nimeshawahi kwenda mganga
zamani sana, ni miaka imepita na sababu ya kwenda haikuhusiana na muziki
bali maisha yangu binafsi, kwenye maisha ya uswahilini ni vitu vingi
vinatokea na ilikua ni ushawishi wa watu wengine…. sikupewa dawa wala
sikuchanjwa taratibu za mganga zilinifanya nisifikie huko‘
‘Kwenye akili ya kujitambua
unaambiwa vitu vingi kama kijana au mtu anaetafuta maisha unaweza
ukachanganywa na vitu vingi sana lakini nakwambia Mungu ni wa ajabu
sana, miaka ambayo nilikwenda kwa Mganga nilikua bado sijaiachia ‘sikati
tamaa’ na sikuwahi kufanikiwa‘ – Darassa
Hapa ni video ya mazungumzo na mwandishi
chanzo:milardayo.com
0 comments: