Ujenzi wa Ikulu ya rais wa Burundi kukamilika mwaka huu
Mradi huo utaboresha mazingira ya kikazi ya viongozi wa Burundi, kuchangia maeneleo ya uchumi wa sehemu zilizo karibu na kuwa alama ya taifa hilo.
Mradi huo unaofanywa kwa msaada wa serikali ya China, uko kaskazini mashariki mwa Bujumbura, mji mkuu wa Burundi, na umetoa nafasi za ajira kwa watu mia tatu nchini humo, ambao wamepewa mafunzo ya kiufundi kwa nusu mwezi na zaidi kabla ya kuanza kazi.
Kansela wa uchumi kwenye ubalozi wa China nchini Burundi Lu Jun amesema, China na nchi za Afrika zinapaswa kutendeana kwa udhati wa moyo, na kwamba China ina uzoefu wa kutosha katika kujiendeleza, na inapenda kusaidia nchi za Afrika kupata maendeleo
Chanzo: http://swahili.cri.cn/
0 comments: