Waachiliwa kuhusu kosa la fidia Libya
Maafisa wawili, wa Libya
wameachiliwa, katika kesi iliyokuwa inawakabili ya kufuja pesa za umma
kwa kukubali kuwalipa fidia waathiriwa wa shambulizi la ndege katika
anga ya Lockerbie mwaka 1988.
Kesi dhidi ya waziri wa zamani wa mambo ya nje
Abdelaaty al-Obeidi na mkuu wa baraza la Congress Mohamed al-Zway
wamekuwa ,imekuwa ikisikilizwa tangu mwaka 2012.Hii ndiyo hukumu ya kwanza kutolewa dhidi ya maafisa wakuu tangu kuuawa kwa Gadaffi.
Jaji hakuelezea sababu za kuwaachilia huru wawili hao , kulingana na mwandishi wa BBC Rana Jawad mjini Tripoli.
Mmoja wa jamaa za al-Zway, aliambia BBC kuwa hii ni ishara tosha kwamba Libya ina mfumo huru wa kisheria.
''Nina furaha sana na idara ya mahakama kuwa nilikuwepo wakati hukumu ikitolewa,'' alisema jamaa huyo.
chanzo:bbc swahili
0 comments: