Mapendekezo 9 ya Wazanzibar
Kamati ya Maridhiano ya Kisiasa Zanzibar inayoongozwa na mwanasiasa
mkongwe, Mzee Hassan Nassor Moyo, imeyataja mambo tisa ambayo
yanastahili kujumuishwa katika katiba mpya ili kuondosha malalamiko
ndani ya muungano.
Wakati Rasimu ya Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
ikitarajiwa kutangazwa wakati wowote mwezi ujao, Kamati ya Maridhiano ya
Kisiasa Zanzibar inayoongozwa na mwanasiasa mkongwe, Mzee Hassan Nassor
Moyo, imeyataja mambo tisa ambayo yanastahili kujumuishwa katika katiba
mpya ili kuondosha malalamiko ndani ya muungano. Mambo hayo ni pamoja
na jina la Jamhuri ya Tanzania kuwa Jamhuri za Tanzania, ufafanuzi
kuhusu jeshi la Polisi; maliasili ya mafuta na gesi asilia, suala la
sarafu, miongoni mwa mambo mengine. Kusikiliza mahojiano ya Sudi Mnette
na Naibu wa Katibu wa Kamati hiyo ya Maridhiano, Eddy Riamy, bonyeza
alama ya kusikiliza masikioni hapo chini.
Mwandishi: Sudi Mnette
Mhariri: Mohammed Khelef
chanzo:dw swahili
Mwandishi: Sudi Mnette
Mhariri: Mohammed Khelef
chanzo:dw swahili
0 comments: