...................
Je wanatibu kweli au wanacheza kamari na maisha ya watu?
Watu wengi nchini Tanzania - na
kote barani Afrika, hutafuta ushauri wa waganga wa kienyeji wanaotibu
maradhi mbali mbali na kupiga kamari.Sheria za serikali na madawa ya
kisasa, huenda zimebadilika , lakini waganga wa kienyeji wangalipo tena
kwa sana. Mpiga picha Sasja van Vechgel alikutana na baadhi yao. Mganga
huyu anaendesha kazi yake katika 'Kitala', kijumba kidogo anachotumia
kuwapa wagonjwa dawa
Baadhi ya watu kuonelea bora
kutibiwa na daktari wa kienyeji kuliko daktari wa kawaida kwa kuwa na
umani nao zaidi na labda kutokana na madawa ya kisasa kukosa kufanya
kazi
Wanawake na wanaume wanaweza kuwa
waponyaji, inategemea tu umri. Wale wanaoheshimiwa zaidi ni wale ambao
jamaa wao mmoja amewahi kuwa mganga. Mwanamume huyu mwenye umri wa miaka
40 anasema yeye anawatibu wanaopooza. Yeye ni kama mchuuzi akitembeza
dawa zake nyumba hadi nyumba. Wakati mwingine hutumia chumba cha
hospitalini kuwatibu wagonjwa wake, ingawa hakuna thibitisho la
kisayansi kuwa dawa zake zinaponya
Matibabu hujumuisha mchanganyiko
wa matambiko na dawa za kienyeji.Waganga wanasema kuwa wanaweza kufanya
kazi yao kutokana na mwongozo wa wazee wa jadi ikiwa wamepagawa na pepo .
Wao hutumia mboko wakitoa matamshi yasiyoeleweka
''Chupa hii ndio kifaa muhimu kwangu,'' anasema mganga huyu mwenye umri
wa miaka 88.
Mgonjwa huyu ametibiwa kwa
ugonjwa wa mifupa.Waganga hutumia majani au migomba ya miti inayotolewa
kwa miti yenye uwezo wa kutibu. Wao huikoroga kwa pamoja na kisha
kuisugua mgongoni au sehemu anayoumwa mgonjwa
Baadhi ya waganga huuza vifaa
mbali mbali kama pembe za wanyama. Matibabu ya waganga hawa inaweza kuwa
kati ya dola 5 au nane na wakati mwingine hata miamoja kulingana na
ugonjwa
Baadhi ya waganga Kusini mwa
Tanzania husema kuwa dawa huwa na nguvu zaidi ikiwa na sehemu ya mwili
wa mtu mfano wale walio na ulemavu wa ngozi au Albino
Baadhi ya wagonjwa ambao huja
kwangu tayari wamekwenda hospitalini bila mafanikio. Sindano na madaya
hayajaweza kuwatibu. Mganga huyu anasema kuwa ikiwa ataweza kumtibu
mgonjwa vyema, habari itawafikia wagonjwa wengine. yeye hana mabango ya
kutangaza kazi yake
Miongoni mwa waganga kuna
misimamo tofauti kuhusu maradhi ya ukimwi. Sio waganga wote wanasema
wana uwezo wa kutibu HIV, lakini mganga huyu ni mmoja wa wale wanaotibu
ugonjwa huo. Anasema kuna wale wanaowashauri wagonjwa kwenda hospitalini
kwa matibabu.
Chanzo:bbcswahili
GIVE YOUR OPINIONS HERE
0 comments: