Je huu ni usajili Bora Ligi Kuu Tanzania?
Wanga, Kaseja na Singano na Usajili 5 bora Ligi Kuu
Tuanze na mabingwa watetezi Yanga ambao ndio waliokuwa wa kwanza kumaliza zoezi la usajili kabla ya siku ya mwisho ambayo ilitangazwa na Shirikisho la soka Tanzania TFF.
Yanga iliamua kutumia kiasi kikubwa cha pesa msimu huu kwa kununua wachezaji watatu wenye majina makubwa Afrika ili kuboresha kikosi chao katika nafasi zilizokuwa zinamapungufu hasa baada ya kuondoka kwa mshambuliaji wake Mrisho Ngassa aliyehamia Free State ya Afrika Kusini.
Donald NgomaUsajili wa mshambuliaji huyo wa kimataifa kutoa FC Platinum ya Zimbabwe ndiyo uliovuma kuliko usajili wa timu zote 16 zinazo shiriki ligi ya Vodacom msimu ujao.
Taarifa zinasema usajili wa Ngoma umeigarimu Yanga zaidi ya Tsh. Milion 93 huku akipokea mshahara wa Dola 4,000 ambazo ni zaidi ya Sh. Milioni 7.9.
Nao washindi wa pili wa Ligi ya Vodacom Tanzania bara Azam baada ya kumrudisha kocha wao Muingereza Stewart Hall nayo ilifanya usajili wa wachezaji wane kuboresha kikosi chao kwa ajili ya kutaka kurudisha taji hilo.
Kati ya wachezaji hao wane iliyowasajili wachezaji wawili ndio usajili wao ulivuta hisia kubwa na kupamba vyombo vingi vya habari ndani ya Tanzania.
Allan Wanga
Ingawa usajili wake ulikuwa wa gafla sana lakini nimoja ya wachezaji waliokuwa wakitajwa na kupambana vichwa vingi vya habari kwenye magezeti ya Tanzania kutokana na uwezo aliokuwa nao wakati akiichezea El Merreikh ya Sudan.
Usajili wa Wanga umefanywa kwa siri kubwa baina ya mchezaji huyo na klabu ya Azam ambayo inasadikiwa mchezaji huyo anapokea mshahara wa Tsh. Milioni 4 baada ya makato ya TRA.
Klabu ya Simba baada ya kuwa na misimu mitatu mibaya nyuma na iliyochangia timu hiyo ikose hata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa msimu huu imeonekana kujipanga kwa kufanya usajili mzuri japo kwa kusuasua.
Abdolaye Pape N’daw
Ndiye aliyefunga zoezi la usajili kwa kikosi cha kocha Dylan Kerr, baada ya kumsajili siku ya mwisho mshambuliaji huyo wa kimataifa kutoka Senegal na hiyo ni baada ya kushindwa kwa wacheza Papa Niang na Makan Dembele raia wa Mali ambao waliletwa kwa ajili ya majaribio.
Nayo klabu changa ya Mbeya City ni moja timu chache zilizongia kwenye orodha ya kutumia kiasi kikubwa cha pesa katika kukiimarisha kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao baada ya kumsajili mmoja ya wachezaji ghali na mkongwe aliyedumu kwenye Ligi ya Vodacom kwa zaidi ya misimu 16 akiwa na timu tofauti.
Juma Kaseja
Klabu ya Mbeya City iliamua kuvunja benki yake msimu huu na kumsajili mkongwe huyo aliyekuwa huru baada ya kuachana na Yanga kwa kushindwa kutimiza masharti yaliopo kwenye mkataba wake ikiwemo kushindwa kumtumia kwenye kikosi cha kwanza.
Usajili wa Kaseja kutua Mbeya City haukutarajiwa kwa kipa huyo aliyekuwa akitajwa kurudi kuichezea timu yake ya zamani Simba lakini gafla Kocha wa Mbeya City Juma Mwambusi akaamua kuvunja benki kwa kutoa Tsh. Million 6 kwa ajili ya kupata saini ya kipa huyo huku wakimlipa mshahara wa milioni 1.5.
Baada ya zoezi la usajili kuongezwa kwa wiki mbili klabu ya Yanga ilifanya mabadiliko kwenye kikosi chake hasa katika upande wa ulinzi baada ya kuonekana kuchoka kwa walinzi wake wa kati Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Kelvin Yondan ambao hawakufanya vizuri sana kwenye michuano ya Kombe la Kagame.
Vicent Bossou
Huyu ni beki wa kimataifa kutoka Togo ambaye amesajiwa kwa mkataba wa miaka mitatu na klabu ya Yanga kutokana na uzoefu aliokuwa nao kwenye michuano ya kimataifa.
Usajili wa Bossou haukutarajiwa lakini kufanya vibaya kwa Cannavaro kwenye kombe la Kagame kulimlazimu kocha Hans van der Pluijm, kuingia sokoni kusaka mbadala wake na kumpata beki huyo ambaye anauzoefu mkubwa kutokana na kucheza mashindano makubwa.
Bossou ameigarimu Yanga kiasi cha Tsh. Milioni 200 na mshahara nakusababisha usajili wake kuwa gumzo ndani ya Tanzania.
Ramadhani Singano
Klabu ya Azam FC chini ya kocha wake Stewart Hall nayo ililazimika kupigana kufa na kupona kuipata saini ya winga Ramadhani Singano ‘Messi’ aliyekuwa na malumbano na klabu yake ya Simba.
Hatimaye alifanikiwa kutua kwenye kikosi cha Azam na kumaliza mjadala na kumzo la muda mrefu kuhusiana na usajili wa mchezaji huyo aliyefanya vizuri akiwa na kikosi cha Simba katika kipindi chote alichoichezea timu hiyo akitokea timu ya vijana.
Haya ndiyo majina ya wachezaji watano ambao usajili wao ulivuma na kuandikwa sana kwenye vyombo vya habari kabla ya dirisha la usajili.
By Zuberi Karim Jumaa
0 comments: