Mheshimiwa Mnyika, amemuomba Waziri Mkuu waliovunja nyumba za King'azi wachukuliwe hatua

...................
post-feature-image


Mbunge wa Jimbo la Kibamba kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika, amemuomba Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, kuwachukulia hatua waliohusika na sakata la kuvunja nyumba  za wakazi wa King’azi kata ya Kwembe Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

 Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mnyika alisema Waziri Mkuu anapaswa kuwachukulia  hatua wahusika kwa kuwa wamekwenda kinyume cha sheria na kusisitiza kuwa anatakiwa kupasua jipu linalopaswa kutumbuliwa kutokana na wananchi hao kuporwa haki zao za msingi. Alisema ukatili huo uliofanywa na watu hao hauwezi kuvumilika kutokana na wananchi hao kuwa katika hali ngumu ya kimaisha, huku wakikosa vyoo, chakula na sehemu za kulala.

“Hili nalo ni jipu, watu wanajichukulia sheria mkononi kwa mgongo wa Mahakama, hivyo Mkurugenzi na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, wanapaswa kujitokeza ili tuwasaidie wananchi hawa,” alisema Mnyika.

Hatua hiyo inatokana na wananchi takriban 269 wa kata hiyo, kukosa mahali pakuishi baada ya nyumba zao 51 kubomolewa na watu zaidi ya 50 wa jamii ya Kimasai waliokuwa wamebeba marungu, mapanga na sime wakishirikiana na Jeshi la Polisi.
-Nipashe
http://3.bp.blogspot.com/-e0QpO-QtZzE/U5DWDUZasXI/AAAAAAAABWg/QlFF97gwNdc/s1600/RAHA+GIF.gif
GIVE YOUR OPINIONS HERE

0 comments: