VIDEO: MAJIBU YA MKURUGENZI WA SHIRIKA LA NYMBA JUU YA SAKATA LA MBOWE
Baada
ya Shirika La Nyumba la Taifa kupitia kampuni ya udalali kutoa samani
mbalimbali katika jengo la Club Bilicanas na jengo lenye Ofisi ya Free
Media kufuatia mmiliki wa ofisi hizo Freeman Mbowe kudaiwa kutolipa deni
ambalo ilielezwa kuwa anadaiwa na shirika hilo.
Aidha hivi
karibuni ziliripotiwa habari kuwa Mbowe amesema kinachofanyika ni siasa
kwani wanafanya kama kumkomoa kwa sababu mara zote amekuwa mstari wa
mbele kuikosoa serikali kuhusu hali ya siasa nchini.
Leo
September 04 2016 kupitia kipindi cha funguka kinachorushwa na kituo cha
television cha Azam Tv, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu amejibu madai hayo kwa kusema……..
>>>’National
Housing ninayoiongoza mimi haijawahi kusukumwa kwa mkono wa siasa, na
tungekuwa tumesukumwa na mkono wa siasa tusingefanya haya tuliyoyafanya
kwa muda mfupi, taasisi za serikali zimeshagusa machungu yetu, hata
chama tawala idara yake makao makuu‘
Unaweza kuangalia video hii hapa chini
chanzo: http://millardayo.com/nhc45

0 comments: