Unawafahamu Wachezaji watano wa kuchungwa kwenye kikosi cha Azam FC msimu wa 2015/16?
Goal inakuletea wachezaji watano wa kuchungwa kwenye kikosi cha Azam FC msimu huu 2015/16
1.Farid Mussa Maliki
1.Farid Mussa Maliki
Chipukizi mwenye thamani ya Tsh. Milioni 20 aliyepo kwenye kikosi cha
kwanza cha kocha Stewart Hall ambaye baada ya kuandamwa na majeruhi ya
muda mrefu msimu huu ameonekana kuwa na kasi ya ajabu na kutarajiwa kuwa
na mchango mkubwa kwenye timu hiyo.
Baada ya kufanya vizuri kwenye michuano ya Kombe la Kagame ikiwepo
bao lake zuri kwenye mchezo wa nusu fainali dhidi ya KCCA, ya Uganda na
kufanya vizuri kwenye pambano la Ngao ya Jamii dhid I ya Yanga Maliki
ameonyesha kuwa ni mchezaji wa kuchungwa na atakuwa na msaada mkubwa kwa
kikosi cha Azam msimu huu.
2.John Bocco
John Bocco mshambuliaji kipenzi cha kocha Stewart Hall wa Azam
amekuwa kwenye kiwango cha juu hivi sasa na ni mmoja ya wachezaji hatari
na ghali walipo kwenye kikosi cha mabingw hao wa Kombe la Kagame.
Bocco anahitaji kuwekewa ulinzi mkali na mabeki wa timu pinzani
kutokana na mshambuliaji huyu mrefu kulijia vuzri goli kila anapopata
nafasi ya kuweza kufunga uwezo aliouonyesha kwenye michuano ya Kombe la
Kagame niwazi anaonekana kuwa na mchango mkubwa kwenye timu yake pindi
ligi ya Vodacom itakapoanza hivi karibuni.
3.Kipre Tchetche
Mshambuliaji hatari wa Azam FC inatarajiwa kuwa na mchango mkubwa kwa
timu yake kwenye msimu unaokuja wa 2015/16 kutokana na kurudi kwenye
kiwango chake baada ya kuuguza majeruhi ya muda mrefu kitu kilichomfanya
afanye vibaya msimu uliopita.
Tchetche raia wa Ivory Coast anafanya vizuri kwenye mechi mbalimbali
za kirafiki na kuisaidia timu hiyo kupata matokeo mazuri na kurudi kwa
kocha Stewart Hall kunaweza kumfanya mchezaji huyo akarududia rekodi
yake ya kuwa mfungaji bora kama alivyofanya misimu mitatu iliyopita.
4.Allan Wanga
Bado hajaichezea timu hiyo hata mechi moja lakini ni mmoja ya
washambuliaji anayetarajia kupewa ulinzi mkali na mabeki wa timu pinzani
kutokana na uwezo wake mkubwa wa kufunga mabao kutokana na uwezo na
nguvu alizokuwa nazo.
Wanga ametua Azam mwezi uliopita akisaini mkataba wa mwaka moja baada
ya kuachana na El Merreikh ya Sudan aliyoichezea kwa mafanikio akitokea
klabu ya FC Leopard ya kwao Kenya.
5.Mudathir Yahya
Huyu ni chipukzi mwengine anayetarajiwa kufanya mambo makubwa akiwa
na kikosi cha Azam FC msimu ujao kutokana na kipaji alichokionyesha
misimu miwili iliyopita na sasa kocha Stewart Hall ameonekana kumuamini
na kumpa nafasi kwenye kikosi cha kwanza.
Muda alifanya vizuri kwenye michuano ya Kombe la Kagame na kuwaweka benchi wakongwe wengi akiwepo Didier Kavumbagu na Amme Ali
0 comments: